Back to top

(TBS) yaendesha zoezi la kukamata nguo za ndani za mitumba Songea

22 May 2019
Share

Shirika la viwango nchini (TBS) limeendesha zoezi la kukamata nguo za ndani za mitumba kwa wauzaji wa nguo za mitumba wilayani Songea mkoani Ruvuma na kusisitiza kuwa nguo za ndani za mitumba zikiwemo sidiria na soksi haziruhusiwi kuuzwa kwa kuwa zina madhara kwa watumiaji.

Zoezi hilo limeendeshwa na (TBS) katika soko la mitumba la Majengo wilayani Songea mkoani Ruvuma na kubaini uwepo wa nguo za ndani za mitumba hasa sidiria na kuzikusanya kwa ajili ya kuzichoma moto ambapo zoezi la kuzikusanya nguo hizo linaendelea na baadaye zitachomwa moto baada ya kukusanywa wilaya zingine za mkoa wa Ruvuma

Kwa upande wao wafanyabiashara wa mitumba wameomba kusamehewa kwa kuwa pesa wanazofanyia biashara ni za mkopo huku pia wakiomba serikali kudhibiti nguo za ndani za mitumba toka zinakotoka.