Maofisa wa shirika la viwango Tanzania, (TBS)wakiongozwa na mkurugenzi wake Dkt. Athuman Yusuph Ngenya wamefanya ukaguzi katika maduka jijini Mbeya na kuchukua baadhi ya bidhaa za ujenzi na vyakula kwenda kuzipima ili kuhakiki ubora wake kwa lengo la kuhakikisha wanadhibiti bidhaa feki na hafifu kuingia sokoni.
.
Aidha Baadhi ya wafanyabiashara wameliomba shirika hilo kuendesha ukaguzi wa aina hiyo mara kwa mara ili kutokomeza bidhaa feki sokoni kwa kuwa zinaathari kubwa kwa wauzaji na watumiaji wa bidhaa hizo.