Back to top

TLS CHAGUENI VIONGOZI KUZINGATIA VIGEZO

01 August 2024
Share

 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko, amekitaka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mawakili, kusimamia Haki na Amani nchini, ili kuhakikisha haki inatendeka kwa watu wote ili kuchochea maendeleo.

Dkt.Biteko ametoa wito huo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, kufungua Mkutano  Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanansheria Tanganyika una oendelea Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Mkuu amewataka wajumbe kuchaguana kwa kuzingatia vigezo nia na mwelekeo wa wagombea watakao kiwezesha chama hicho, kusonga mbele na siyo wale wanaotanguliza maslahi binafsi badala ya chama.

Amesema TLS wakati inaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, wanachama wake wanatakiwa kutafakari mwelekeo wa chama hicho kitaaluma, ili kuendana na azma ya serikali ambayo imeweka nia thabiti katika kuhakikisha haki inaonekana ikitendeka.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameipongeza TLS kwa ushirikiano na taasisi za elimu na taasisi rafiki na TLS kuhakikisha Wananchi wanapata haki kwa wakati.