Back to top

MAENDELEO YA MTOTO WA KIKE, ALIKIBA ATWAA TUZO

20 October 2024
Share

Msanii wa BongoFlava Ali Kiba ametunukiwa Tuzo kama Champion wa Maendeleo ya Mtoto wa Kike, kupitia Kongamano la Kigoda cha Wasichana, lililofanyika katika siku maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Kike visiwani Zanzibar. 

Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Shiraz Foundation. Alikiba amekabidhiwa tuzo hiyo alipohudhuria na kushiriki Kongamano hilo viwanja vya Nyamanzi Zanzibar, na Mgeni Rasmi alikuwa Mh. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (SMZ) Riziki Pembe, Mgeni Maalum na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Zena Said na Mgeni Maalum na Mlezi wa Jukwaa hilo Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Bi Mgeni Juma. 

Kwa upande wake Alikiba amepongeza Jukwaa hilo la Kigoda cha Wasichana na kuahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika mambo mengine ya Kijamii na kuendelea kumuwezesha Mtoto wa Kike.