Back to top

TMA: TANZANIA HAMTAONA KUPATWA KWA JUA

08 April 2024
Share

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA), imesema Tanzania haitashuhudia tukio la kupatwa kwa jua, linalotarajiwa kutokea leo Aprili 08, 2024, kwa sababu iko eneo la mbali zaidi na njia ambayo hali hiyo itatokea.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imeeleza kuwa hali hiyo itatokea upande wa Bara la Amerika ya Kaskazini kupitia Mexico, Marekani na Kanada na kwamba linatarajiwa kuanzia maeneo ya kusini mwa Bahari ya Pasifiki ambapo Mexico itakuwa nchi ya kwanza kufikiwa.