Back to top

Tozo ya Sh. 1,000,000/= kwa magari ya Misiba yapingwa Arusha.

18 January 2021
Share

Tozo mpya ya shilingi milioni  moja kwa magari yanayokodishwa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo  ya kubeba  miili  ya marehemu inayosimamiwa na (LATRA) imepingwa  na wadau  wa  usafirishaji  jijini Arusha   ambao  wameiomba serikali kuangalia upya suala hilo.
.
Mjadala huo umeibuka kwenye  kikao cha watendaji  wa LATRA na wadau  hao ambao wamewalalamikia  watendaji  wa idara zinazosimamia biashara hiyo ikiwemo LATRA kuwa zinaendelea kuwakandamiza badala ya  kuwasaidia.
.
Meneja leseni kutoka Mamlaka Ya Udhibiti Usafiri Wa Ardhini (LATRA), Bw.Leo Ngowi na  mkurugenzi wa huduma za usafiri wa wizara ya ujenzi na uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka wamewataka wafanyabiashara hao kuwa  watulivu  na kuendeea  kutoa  ushirikiano na  mapendekezo kwani  yote yatazingatiwa.
.
Kwa  sasa huduma za magari ya kukodisha yakiwemo yanayobeba watu wanaokwenda kwenye harusi ama kwa shughuli  za  misiba na pia  yanayobeba  miili  ya watu  wanaofariki asilimia kubwa zinatolewa na magari ya kawaida yakiwemo yanayotumka kubeba abiria na mizigo utaratibu ambao sheria hiyo ikipitishwa  hautakuwepo