Twiga adimu zaidi duniani aliyezaliwa bila madoa yoyote katika Bustani ya Wanyama ya Brights huko Limestone, Tennessee, Julai 31, mwaka huu na kuwa gumzo huku ikiaminika kuwa pekee wa aina yake duniani .
Alizaliwa tarehe 31 Julai katika Bustani ya Wanyama ya Brights huko Limestone, Tennessee, ni twiga mchanga ambaye ana urefu wa futi sita, na urefu wa wastani wa kuzaliwa wa twiga jike ni kama mita 1.8 (futi 6).
Shirika la Uhifadhi wa Twiga (GCF) limesema Twiga huanza kunyonya maziwa ya mama yake punde tu wanapoweza kusimama - ndiyo maana wanahitajika kuwa warefu sana wanapozaliwa.
Ndama hutegemea maziwa ya mama yao kwa muda wa hadi miezi 9-12. Wanaanza kula chakula kigumu (majani) kuanzia miezi 4 wanapokuwa na uwezo wa kutafuna.