Back to top

Ufafanuzi kuhusu kifo cha muuguzi wa hospitali ya Taifa Muhimbili.

19 April 2020
Share

Kuna taarifa inasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa Marehemu Evodia  Kapinga amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona na kwamba alikua akihudumia wagonjwa wa Corona.

Marehemu Kapinga hajawahi kuhudumia wagonjwa wa wanaougua ugonjwa wa Corona.

Marehemu alikua akitoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto. 

Marehemu ni mgonjwa wa siku nyingi aliyekua akisumbuliwa na MARADHI AMBAYO HATUWEZI KUYATAJA KULINGANA NA MAADILI YA TIBA.


Jana jumamosi tarehe 18 Aprili, 2020 saa NNE USIKU marehemu akiwa nyumbani kwake Kimara, alizidiwa ambapo watoto wake walifanya jitihada ya kumkimbiza Muhimbili lakini wakiwa njiani hali yake ilibadilika ndipo walipompeleka Hospitali ya karibu ya Sinza, Palestina.

Madaktari na Wauguzi walifanya kila jitihada kuokoa maisha yake bila mafanikio ambapo amefariki leo jumapili saa 09 alfajiri.


Hivyo, taarifa  zinazosambaa kuwa kifo chake kinatokana na ugonjwa wa Corona siyo za kweli, ZIPUUZWE.