Back to top

UGANDA: LORI LA MAFUTA LALIPUKA, WATU 11 WAFARIKI

23 October 2024
Share

Watu Zaidi ya 11 wamefariki dunia, baada a lori la mafuta, kupinduka na kulipuka karibu na mji mkuu wa Uganda, Kampala, baada ya lori hilo kupoteza muelekeo kutokana na hitilafu ya breki.

Msemaji wa Polisi nchini humo, Patrick Onyango amesema kulipuka kwa lori hilo baada ya ajali kati ya watu 11 waliofariki wawili miongozni mwao ni Watoto na kwamba wathiriwa waliteketea bila kutambuliwa kufuatia mlipuko huo wa lori.

Onyango ameeleza kuwa licha ya tahadhari wanaozito panapotokea matukio ama hayo, lakini bado watu walionekana wakisogea maeneo ayo kwa lengo la kuchotamafuta, ambapo tukio ama hilo lilitokea nchini Nigeria na kuua zaidi ya watu 140 wakiwemo watoto.