Back to top

Ugonjwa wa Macho na shinikizo la damu changamoto Mto wa Mbu.

08 April 2019
Share

Madaktari bingwa kutoka hospitali za serikali na binafsi wametoa matibabu na vipimo bure kwa mamia ya wakazi wa mji wa Mto wa Mbuu, wengi wao kutoka familia zisizo na uwezo na kubaini idadi kubwa wanasumbuliwa na na magonjwa ya macho na shinikizo la damu kutokana na mazingira wanayoishi.

Wakizungumza na ITV, baadhi ya waliopatiwa huduma hizo, wamesema zimekuja wakati muafaka kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kifedha kugharamia matibabu ndiyo maana maradhi hayo yamewaandama kwa muda mrefu.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Kirurumo kinachohudumia eneo hilo amesema idadi kubwa ya waliopatiwa matibabu wamegundulika kuwa na magonjwa kwa kuwa hawana utamaduni wa kukagua afya zao.

Mratibu wa matibabu hayo kutoka Klabu ya Lions Bwana Masanya amesema klabu hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuguswa na hali za wakazi hao na kwamba waliyogundulika kuathirika zaidi watapatiwa rufaa na huduma ya bure ya upasuaji.