Back to top

UKAUSHAJI DAGAA KWA VICHANJA WAMKOSHA ULEGA

23 September 2024
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega, amewatembelea wavuvi wa Ziwa Nyasa, na kukagua shughuli mbalimbali wanazozifanya, ikiwemo ukaushaji wa dagaa kwa kutumia vichanja, na sio kuanika chini kama ilivyokuwa zamani.

Katika ziara yake hiyo, Waziri Ulega, amefurahishwa kuona wavuvi hao wakitumia njia ya uongezaji thamani wa zao la dagaa, kwa kuwakausha kwa kutumia vichanja, mfumo ambao unasaidia dagaa kuwa bora.

Waziri Ulega amewapongeza wavuvi na kuwaeleza kuwa, serikali imedhamiria kuboresha shughuli zao na ndio maana imekuwa hatua kwa hatua ikiwawezesha kwa elimu, kuwapatia vifaa na zana za kisasa za uvuvi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Nyasa, Mhandisi Stella Manyanya, amemshukuru Waziri Ulega, kwa kuwapa elimu wavuvi hao juu ya namna bora ya uchakataji wa zao la dagaa, na ndio maana sasa wanawaanika kwenye vichanja na sio chini tena kama zamani.