Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Abdallah Ulega, ameweka jiwe la msingi wa ujenzi wa Daraja la Kigonzile mkoani Iringa, ambapo kabla ya ujenzi wa daraja hilo wananchi walikuwa wanapata tabu kutoka sehemu moja kwenda upande mwingine kufanya shughuli zao za kila siku.
"Ujenzi wa daraja hili ni uthibitisho kwamba Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya kazi kubwa ya kutatua kero za wananchi, tunamshukuru sana Mhe. Rais"-mesema Ulega
Ameipongeza TARURA kwa kufanya kazi nzuri ya ujenzi wa Daraja hilo, ambalo litasaidia wananchi kufanya shughuli zao vyema.
Naye, Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe.Jesca Msambatavangu, amesema daraja hilo lililojengwa kwa gharama ya shilingi Milioni 119, ni muhimu sana kwao kwa linakwenda kutatua kero ya mawasiliano kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
"Sisi wananchi wa kata ya Nduli tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea daraja hili na sasa tunaamini kazi zetu zitaendelea, uchumi wetu utakuwa na maisha yatabadilika"Amesema Msambatavangu