Back to top

Utafiti wabaini Ruvuma Ina miamba yenye Chuma na Shaba.

18 May 2019
Share

Katibu mkuu wizara ya madini Prof Simon Msanjila amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na nchi ya Korea kupitia mradi wa majaribio wa nchi za Afrika katika mkoa wa Ruvuma umebaini baadhi ya maeneo ya mkoa huo uwepo wa miamba yenye madini aina ya chuma na shaba kwenye tabaka la juu la ardhi.

Akizungumza wakati akipokea ripoti ya utafiti huo jijini Dodoma.Prof. Msanjila amesema pia taarifa zilizochukuliwa na ndege zinaonyesha kuwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Ruvuma yana miamba yenye usumaku mkubwa, ambAyo inaweza kuashiria uwepo wa madini ya chuma na madini mengine .

Kwa upande wake Kaimu mtendaji mkuu wa wakala wa jiolojia Tanzania Bi. Augustine Rutaihwa amesema kupitia utafiti huo utawezesha wakala wa jiolojia kuendelea kugundua maeneo mbalimbali yenye madini kwa maslahi ya taifa huku akisema kuwa utafiti huo ni endelevu katika maeneo mengine hapa nchini.

Hata hivyo katika utafiti huo taarifa za jiolojia katika maeneo ya Ruvuma, ambayo ni kwenye mpaka wa Msumbuji na Tanzania pamoja na Tunduma kwenye mpaka na Zambia zimeboreshwa kuwa za kisasa zaidi zikihusisha kutafuta uhusiano wa jiolojia kwenye maeneo ya mipaka.