Madaktari bingwa na Bingwa Bobezi, wapatao 64 wa Mama Samia, walioanza kambi mkoani Mtwara, wametakiwa kuwa chachu ya huduma bora za afya kwa siku zote tano, watakazoweka kambi mkoani humo.
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dkt. Denedicto Ngaiza, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bahati Geuzye, wakati wa ufunguzi wa Kambi ya awamu ya pili ya Madaktari bingwa na Bobezi iliyopo mkoani humo.
“Mbali ya jukumu kubwa mlilonalo lakutoa huduma kwa wanaanchi, tumieni fursa hii pia kuwajengea uwezo wataalamu wenzenu katika ngazi ya msingi ili kuhakikisha wananchi wa ngazi ya msingi wanapata Huduma bora, stahiki na kwa wakati”, amesisitiza Dkt. Ngaiza.
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi Afisa Programme kutoka Wizara ya Afya, Celphlen Budodi, amesema huduma zitakazotolewa na Madaktari bingwa ni pamoja na magonjwa ya watoto, wanawake na uzazi, kinywa na meno, dawa za usingizi na ganzi, uuguzi na ukunga, magonjwa ya ndani, upasuaji na njia ya mkojo, pamoja na mifupa na kwa hospitali ya Manispaa ya Mikindani Mtwara.
" Wakati wa zoezi hilo wananchi wameombwa kuchangia gharama kiasi huku akisisitiza wenye bima za afya kuwa nazo kwaajili ya kupata matibabu hayo kutoka kwa madaktari bingwa na bingwa bobezi" amesema Budodi
Kwa upande wao Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka hospitali ya Perahimo mkoani Ruvuma, Dkt. Monica Mboka amesema kuwa huduma hiyo wanaitoa kwa mara ya pili ikiwa ni muendelezo uliosukumqa na mwamko wa awamu ya kwanza.
Naye Daktari Bingwa wa upasuaji toka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dkt. Dino Simoni amewahaidi wananchi kutoa huduma bora huku akiweka bayana kuwa watakuwa na madaktari bingwa wa mgonjwa ya meno ambapo hapo awali hawakuwepo.
Madaktari Bingwa wa Mama Samia watakuwepo kwenye mkoa huo kwa muda wa juma zima ikiwa ni muendelezo wa kambi iliyofanyika mapema mwezi Mei hadi Juni, 2024.