Back to top

Vifo kutokana na majeruhi wa ajali ya Lori na Basi Moro vyafikia 94.

17 August 2019
Share

Idadi ya vifo vya ajali ya lori la mafuta lililopinduka na kuwaka moto mkoani Morogoro imeongezeka na kufikia 94 baada ya majeruhi mwingine mmoja kufariki wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha Wakati akipokea msada wa damu uniti 100 kwa ajili ya Majeruhi wa Ajali hiyo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, na kusema kwa sasa majeruhi wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamebaki 20. 

Taarifa ya Habari ya Asubuhi Agosti 17, 2019