Back to top

Vifo vya majeruhi ajali ya Moto Morogoro vyafikia 100.

21 August 2019
Share

Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam Dkt. Lauriane Rwenyuma amesema wagonjwa walioungua baada ya lori la mafuta kuwaka moto mkoani Morogoro waliungua kwenye mapafu na hata kusababisha upumuaji wao kuwa washida.

"Wengi waliungua kwenye mapafu kwa maana hata upumuaji wao ulikuwa sio mzuri wanatumia mashine, kwasababu hawawezi kupata Oksijeni ya kutosha".Rwenyuma-Bingwa wa upasuaji Muhimbili.

Rwenyuma ametoa kauli hiyo leo Agosti 21, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuwaeleza hali za majeruhi na hatua wanazoendelea nazo ili kuhakikisha kwamba afya zao zinaimarika.

Amesema kwa sasa wanachofanya kwa majeruhi waliobaki ni kwamba sehemu walizoumia kwenye miili yao, wanajaribu kuitibu kiiutaalam ili kuahakikisha wanafunika jeraha lililopo.

"Na operesheni inayohitajika ni ya kufunika jeraha la moto, sasa akibahatika kama kuna ngozi iliyobaki basi ndio huwa tunachukua na tunaibandika kwenye lile jeraha".Rwenyuma-Bingwa wa upasuaji Muhimbili. 

Aidha leo Agosti 21, 2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitali ya Muhimbili, Aminieli Aligaesha alitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya majeruhi watatu waliokuwa wakipatiwa matibabu hospitalini hapo, ambapo mpaka sasa idadi ya waliofariki kutokana na ajali hiyo ya moto imeshafika 100 huku 15 wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya Muhimbili.