Back to top

Vipimo vya homa ya Dengue sasa ni bure

21 June 2019
Share

Serikali imesema kuanzia sasa vipimo vya homa ya dengue vitatolewa bure kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya umma kwa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa huo.

Aitoa kauli ya serikali bungeni kuhusu mlipuko wa homa ya dengue hapa nchini,waziri wa afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu mbaka sasa jumla ya wagonjwa  elfu 4,320 na vifo vinne vilivyotokana na homa ya dengue vimetolewa taarifa huku mkoa wa Dar es Salaam ukiwa unaongoza.

Amesema serikali itaboresha matibabu kwa wagonja kwa kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa dawa za kutosha na pia itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa afya sambamba na kuboresha mifumo ya ukusanyaji takwimu.

Mhe.Mwalimu amesema katika kukabiliana na ugonjwa huo,serikali imenunua kiasi cha lita elfu 60 za viuavidudu kwa ajili ya kuangamiza viliwiluwi katika mazalia ya mbu.

Amesema kati ya lita hizo lita elfu 11,400 zimesambazwa kwenye halmashauri tano za mkoa wa Dar es Salaam, na lita elfu 48 zinasambazwa kwenye halmashauri za mikoa ya GeitaKkagera,Kigoma,Lindi na Mtwara na lita zaidi ya elfu 36 zitasambazwa katika mikoa mingine.

Akizungumzia changamoto za udhibiti wa ugonjwa huo Mhe.Mwalimu amesema licha ya serikali kununua vipimo vya ugonjwa huo na kuviuza kwa bei nafuu bado wananchi wengi wameshindwa kumudu gharama za uchangiaji matibabu ya ugonjwa huo.

Amesema ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unadhibitiwa mikoa yote nchni na halmashauri zote nchini hasa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya dengue na malaria kusimamia kikamilifu kampeni za usafi wa mazingira na kuangamizi mbu kwa kunyunyizia  dawa.