Serikali imeliambia bunge, kuwa imeanza mkakati wa kujenga vituo vya polisi, katika kila kata hapa nchini.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Jumanne Sagini, amesema hayo bungeni mkoani Dodoma, wakati akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake.
Naye Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson, ameitaka wizara hiyo kujenga makazi ya askari polisi nchi nzima, kitu ambacho kimekuwa changamoto kwao.
Mkutano wa kumi na tatu wa bunge unafikia tamati leo mkoani Dodoma.