Back to top

Wagonjwa wasota kwa zaidi ya saa nane bila kupata huduma Musoma.

05 February 2019
Share

Upungufu wa wauguzi na madaktari katika kituo cha afya cha Nyasho katika halmashauri ya manispaa ya Musoma mkoani Mara,umesababisha wananchi kuchukua zaidi ya saa nane hadi kumi kupata huduma za matibabu,hatua ambayo imetajwa kuwa kero kubwa kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho.

Wakizungumza  na ITV baada ya kukutwa wakiwa wamekaa kwa zaidi ya saa nane bila kupata huduma katika kituo hicho cha afya baadhi ya wagonjwa wamesema upungufu huo wa madaktari na wauguzi katika kituo hicho umesababisha kero kubwa hata wakati mwingine kusababisha baadhi ya wagonjwa kufariki dunia kabla ya kupata matibabu hivyo wameiomba serikali kupitia wizara ya afya kuchukua hatua ya kutatua changamoto hiyo.

Hata hivyo Mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Musoma Dk Saidi Mauji amekiri kituo hicho kukukabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari na wauguuzi ukilinganisha na idadi kubwa ya wagonjwa inayopokelea kutoka ndani ya halmashauri ya manispaa hiyo na vijiji jirani vya wilaya za Musoma,Butiama na Rorya.