Back to top

Wakazi wa Nambaya,wilayani Masasi wanakunywa supu ya ngozi.

16 May 2018
Share

Kukosekana kwa maduka ya nyama katika kijiji cha Nambaya wilayani Masasi na mkoa wa Mtwara kumesababisha wakazi wa eneo hilo kuchemsha ngozi na kula kama supu kwa kile walicho kidai ni uhaba wa mifugo licha ya ngozi hizo kutegemewa kama malighafi ya viwanda kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu na mikanda.

ITV imetembelea katika vijiji mbalimbali ya wilaya hiyo nakushuhudia wananchi wakila ngozi hizo kama supu ambapo mbele ya kamera ya ITV wamesema kukosekana  kwa nyama katika eneo hilo ndio sababu ya kuwafikisha hatua hiyo.

Kwa upande wake mama lishe ambaye ni muuzaji wa supu hiyo Dafroza Joseph amesema analazimika kufuata ngozi hiyo umbali mrefu huku akiuziwa seti ambayo ni muunganiko wa ngozi,makanyagio na kichwa kwa shilingi laki moja na hamsini.

ITV ikamtafuta afisa mifugo wa wilaya hiyo Rioba Mgabe ili kufahamu undani wa swala hilo ambapo amesema wananchi hao wamekuwa wakila ngozi hizo kwa muda mrefu huku akisema ng’ombe wanaochinjwa wilayani hapo wanakidhi mahitaji na bado wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuachana na dhana hiyo.