Back to top

WAKOMBOENI WANANCHI NA RIBA TATA.

28 August 2024
Share

Kufuatia kuwepo kwa idadi kubwa ya watoa huduma wanaotoza riba kubwa kwenye mikopo, ambayo wakati mwingine inazidi kiasi cha mkopo huku Taasisi zingine kati ya hizo zikiwa hazijasajiliwa wito umetolewa kwa wizara ya fedha kuongeza nguvu ya kumwakomboa wananchi na mikopo ya aina hiyo.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Bi. Ruth John ambaye amesema wapo baadhi ya wakopeshaji wanawafuata wananchi majumbani na kuwakopesha kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

Bi. Ruth ameyasema hayo alipokutana na Timu ya program maalum ya elimu ya fedha kwa umma kutoka Wizara ya Fedha ofisini na kuongeza kuwa kilio hiki sio tu kwa wajasiriamali bali hata kwa Watumishi wa Umma.

"Changamoto tunazipata sana hadi kwa watumishi wa umma hususan walimu ambao wanaingia kwenye changamoto hiyo kwa sababu kila mtu ana uhitaji wake, na anapopata shida haaangalii kitu gani kipo mbele yake ambacho kitamletea madhara" Alisema Bi. Ruth.