Wizara ya elimu na TAMISEMI,ikishirikiana na wadau wengine, wameanzisha vitengo vya kuwasaidia walemavu viziwi, wasioona ili kujikimu kiuchumi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Sense Bw. Geoffrey Atieli ametoa takwimu ya vijana 17 tu, waliopatiwa mlioni moja kwa kila mmoja kufanya miradi watakayoipenda pia ameiomba jamii iwape ushirikiano mzuri ili kuwasadia walemavu viziwi wasioona katika miradi yao.
Kwa upande wake mwalimu Henry Paul amesema,kuna uhaba wa wataalamu wa lugha ya alama mguso ivyo kupelekea kuwa na changamoto kubwa katika sekta ya elimu.
Naye mwanafunzi Mwanaasha Abdallah, ameiambia ITV kuwa, kutokuwepo kwa nyenzo nzuri za mawasiliano wamekuwa wakipata changamoto katika shughuli zao za kijamii.