Back to top

Wanafunzi 14,046 waliofaulu darasa la saba wakosa nafasi Kagera.

17 December 2018
Share

Jumla ya wanafunzi 14,046 waliofaulu mtihani wa darasa la saba katika mkoa wa Kagera kwa mwaka 2018 kati ya wanafunzi 39,545 waliofaulu mtihani huo hawakupata nafasi ya kuchanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa.

Afisa elimu katika mkoa wa Kagera Aloyce Kamamba  amesema katika kukabiliana na tatizo hilo serikali katika mkoa huo inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mtihani wao wa darasa la saba mwaka 2018 wanajiunga na kidato cha kwanza mwezi Januari mwaka ujao.