
Zaidi ya wanafunzi elfu moja na mia moja waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari mwaka huu katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
Afisa elimu, vifaa na takwimu katika wilaya ya Uvinza Ayada Kalinga amesema hadi sasa wanafunzi elfu tatu kati ya zaidi ya elfu nne ndio wameripoti hivyo jitihada zinafanywa sasa kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuwasaka wanafunzi na wazazi wao ili wanafunzi hao waweze kupata haki yao ya kusoma
Kwaupande wake diwani wa kata ya Uvinza Aloca Mashaka akizungumza baada ya kupokea msaada wa saruji na vifaa vya ujenzi kutoka kampuni ya Nyanza salt mine amesema kuwa kata hiyo imeanza mchakato kwa kushirikiana na wananchi kuongeza miundombinu ya shule ya sekondari Ruchugi ili kuwezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo badala ya kusubiri kukamilika kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa.