Back to top

WANANDOA MATATANI KIFO CHA MTOTO KENYA.

03 October 2023
Share

Kwa mujibu wa majirani, wanandoa hao walianza kumpiga mtoto huyo baada ya kukataa kula Jumatatu jioni, na mama anayemlea mtoto huyo ni mama wa kambo na mama wa mtoto alishafariki.

Walioshuhudia wanasema mtoto huyo ambaye alikuwa na michubuko kwenye mwili wake, alikuwa amekimbizwa katika zahanati iliyo karibu, kisha alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mama Lucy, lakini alifariki kabla ya kufika hospitalini.

“Walimpiga mtoto kwa kukataa kula. Haikuwa mara ya kwanza kufanya hivyo,” Gladys Wamboi, jirani wa wanandoa hao.

Wanandoa hao wanashikiliwa na Polisi na uchunguzi unaendelea kubaini chanzo kikuu cha tukio hilo.