Wananchi wanaojihusisha na uvunaji wa mazao ya misitu ikiwemo Mbao pamoja na mkaa wilayani Handeni mkoani Tanga wametakiwa kufuata sheria na kanuni ili kueupuka uvunaji holela unaofanyika sasa wanaojihusisiha na uvunaji wa mazao ya misitu watakiwa kufuata sheria
Kauli hiyo imetolewa na meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania wa wilaya ya Handeni baada ya wananchi wa vijiji vya Madebe na Mbamba kata ya Kang,ata kulalamikia hali inayojitokeza ya uvunaji wa mazao hayo ya misitu kiholela.
Hali hiyo ndio iliopelekea meneja wa TFS wilayani hapa kufunga safari na kwenda kwenye maeneo yaliotokea uharibifu huo na kukamata zaidi ya gunia mia moja za mkaa huku mmiliki akidaiwa kutokuwa na vibali vinavyo mruhusu kuchoma mkaa katika eneo hilo.