Back to top

WANAOTOA DAWA BILA CHETI CHA DAKTARI KUSHTAKIWA

17 November 2023
Share

Serikali imewaonya Wafamasia na Wamiliki wa maduka ya dawa wanaotoa dawa bila kuangalia cheti cha Daktari kwani kufanya hivyo ni kuendeleza tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha afya za watu.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, leo Novemba 17, 2023, wakati akifunga Kongamano la Tatu la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa na kufungua rasmi wiki ya uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa inayoanza Novemba 18 hadi 24, 2023.
.
Waziri Ummy, amesema atatuma timu kufanya kaguzi za kushtukiza kwenye maduka ya dawa, huku akisisitiza kuwa mfamasia atakaebainika kutoa dawa za Antibiotiki bila cheti cha daktari atafikishwa mahakamani na atalipa faini kubwa.