Wakina mama wajawazito wilayani Kilindi mkoani Tanga wamewalalamikia wanaume wanao wapa ujauzito kukwepa kwenda kliniki kupima afya zao kama kanuni zinavyodai hali inayopelekea wakina mama hao kutafuta wanaume wengine kwenda nao kupima ili waweze kupata kadi ya kliniki.
.
Hata hivyo ITV ilimtafuta mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Kilindi Abubakari Makengwa ili kuthibisha swala hilo nae akakiri kuwepo kwa tabia hiyo kwa baadhi ya wanaume.
.
Aidha, Kwa upande wake mganga mkuu wa wilaya Dr Daniel Chochole nae amekiri kuwepo kwa hali hiyo ila amesema wanaendelea kutoa elimu kwa akina baba wenye tabia hiyo.