Back to top

WASHIRIKI IAWP KUPAMBANA CHANGAMOTO AFYA YA AKILI

03 July 2024
Share

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo kwa askari wakike ukanda wa Afrika (IAWP) ambayo yanaendelea Abuja Nchini Nigeria, wamesema kutoka na changamoto kubwa kwa baadhi ya watu wengi wanaokabiliwa na Afya akili, wanakwenda kupambana na changamoto hiyo kutokana mafunzo waliyoyapata.

Akiongea mara baada ya Mafunzo hayo Jijini Abuja Nchini Nigeria, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Mwamini Lwantale amesema mafunzo hayo yamewaongezea maarifa katika utendaji wao wa kazi za kila siku ambapo amebainisha kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati sahihi.

DCP Mwamini amesema kutokana na changamoto kubwa iliyopo ya Afya ya akili kwa baadhi ya watu amebainisha mafunzo hayo yanakwenda kuwa Mwarobaini wa changamoto hiyo huku akiweka wazi kuwa walichojifunza kina kwema kuifanya jamii kuondokana na changamoto hiyo.

Sitafu Sajenti wa Polisi kutoka Nchini Tanzania Caster Amoury amesema mafunzo waliyoyapata yameongeza mbinu ya namna ya kutekeleza majukum yao huku akibainsha kuwa mafunzo hayo yamewaongezea mbinu mpya ya namna kutoa huduma kwa watu wenye changamoto ya Afya ya akili.

Mkaguzi Mkuu wa Polisi kutoka Nchini Ghana CI Beatrice Neemazi amesema kuwa amefurahi kuwepo katika mafunzo ambayo yanakwenda kuimarisha changamoto za watu na Watoto wenye changamoto za Afya ya akili.

Sajenti wa Polisi Happy bundala amebainisha kuwa jamii itegeme kupata msaada Mkubwa kutoka kwao kutokana na mafunzo mazuri waliyoyapata kuhusiana na changamoto ya Afya ya akili.