
Jopo la wataalamu wa Sheria na Haki za binadamu wa Mkoa wa Mwanza wamepewa Mafunzo maalum ya utayari kuelekea uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign MSLAC)
Akizungumza na wataalamu hao wakati wa uzinduzi wa funzo hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Balandia Elikana amesmema kuwa kufanikiwa kwa Kampeni hiyo kunategemea na wataalamu hao kuzingatia mafunzo hayo na kwenda kufanya kazi kwa weledi.
“Kampeni hii itafanikiwa kama sisi sote tuliopo hapa tutatekeleza wajibu wetu kimamilifu na kufahamu nini hasa tunapaswa kufanya, kwahiyo mafunzo haya yawasaidie kuelewa nini mnapaswa kufanya ili kufanikisha adhma ya serikali yetu ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan” Amesema Elikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Haki za Binadamu Bi. Beatrice Mpembo amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia wataalamu hao kupata uelewa wa pamoja juu ya kampeni hiyo na kufikia malengo yaliyotarajiwa
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa Mkoa wa Mwanza inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Februari 18, 2025 katika viwanja vya Furahisha.