![](https://www.itv.co.tz/sites/default/files/styles/large/public/field/image/korosho%2Bpic.jpg?itok=xJ5wGANM)
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geofrey Mwambe ametoa wito kwa watanzania wenye uwezo wa kuendesha viwanda vya kubangua Korosho kujitokeza ili serikali iwape viwanda hivyo vilivyosimama kufanya kazi kwa lengo la kuongeza kasi ya kubangua Korosho.
Bw. Mwambe ametoa wito huo baada ya kutembelea kiwanda cha kubangua Korosho cha Korosho Afrika cha wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kujionea shughuli za ubanguaji Korosho zinavyoendelea ambapo ameridhishwa na kasi ya ubanguaji Korosho unaoendelea kiwandani hapo.
Kwa upande wake msimamizi wa kiwanda cha Korosho Afrika Bw.Issa Kahesa amesema kiwanda hicho kilichotoa ajira kwa wananchi zaidi ya 500 wengi wao wakiwa wanawake kinabangua Korosho kilizokabidhiwa na serikali kwa ubora wa hali ya juu.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Juma Homera amesema kuwa kuna fursa kubwa ya soko la Korosho zenye ubora wilayani Tunduru.
Pamoja na kutembelea kiwanda cha kubangua Korosho Bw. Mwambe pia ametembelea kiwanda cha kukoboa Mpunga kinachomilikiwa na chama cha ushirika wa umwagiliaji wilayani Tunduru.