Watoto 217 yatima na wahitaji wanaolelewa katika kituo cha malezi ya watoto Mwokachi mjini Kigoma, wamepatiwa bima za afya na kikundi cha wanawake cha (EWG) baada ya watoto hao kukosa msaada wa matibabu na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Watoto pamoja na Mkurugenzi wa kituo hicho Zainab Bi.randeka wamesema kituo hicho kilikuwa kinashindwa kutoa huduma stahiki kwa watoto ambao wanalelewa kituoni hapo kutokana na kupungua kwa ufadhili kutoka taasisi mbalimbali.
Mwenyekiti wa kikundi EWG Aisha Salubobo amesema lengo la kutoa kadi hizo ni kuwawezesha watoto kupata matibabu bila malipo huku Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma Dk. Paul Chaote akisema watoto ambao wako katika mazingira hatarishi pamoja na makundi mengine katika jamii wanahitaji kupatiwa kadi za bima za afya ili wawe na uhakika wa matibabu.