Back to top

Watu 4 wafikishwa mahakamani kwa kosa la kuchezea mizani ya Korosho

04 January 2019
Share

Watu wanne wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuchezea mizani za kupimia Korosho kwa lengo la kuwaibia wakulima katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma huku kumi na tisa wakitozwa faini kuhusiana na kosa hilo.

Akizungumza na waandishi wa hahari meneja wa wakala wa vipimo kanda ya kusini Davidi Makungu amesema zoezi hilo la kushtukiza limefanyika katika mikoa hiyo lengo likiwa kuhakikisha Korosho za mkulima hazipotei ama kuliwa na wajanja wachache.

Hata hivyo baadhi ya makarani wa mizani  katika maghala makuu wanasema zoezi hilo la kushtukiza  limesaidia kuondoa wizi unaofanywa na baadhi ya makarani wanaotumia mwanya huo kuwaibia wakulima.

Kwa mujibu wa wakala wa vipimo elimu wanayoitoa kwa wakulima imesaidia kupunguza wizi wa Korosho unaotokana na mizani.