
Umoja wa Mataifa umesema watu milioni 4.4 duniani , hawana uraia wa taifa lolote, ingawa idadi halisi, huenda ikawa kubwa zaidi kutokana na watu hao "kutotiliwa maanani".
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR), limesema kutokuwa na uraia wa taifa lolote, kuna "athari mbaya" huku likitoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la kutengwa kwa watu hao.
UNHCR imesema wakiwa hawatambuliwi kama raia wa nchi yoyote, watu wasio na utaifa mara nyingi haki zao hukandamizwa huku wakishindwa pia kupata huduma za msingi. Watu hao mara nyingi hutengwa kisiasa na kiuchumi na hukabiliwa na vitendo vya ubaguzi, uonevu na unyanyasaji wa aina mbalimbali.
#DW