Back to top

Watu wawili wakamatwa wakiwa na Bunduki mbili mkoani Ruvuma

08 April 2018
Share

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watuhumiwa wawili baada ya kuwakamata  na bunduki mbili zinazodaiwa kutumika kufanyika Ujangili wakiwemo Tembo na Nyati.

Katika tukio  la kwanza kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi anasema wanamshikilia mtuhumiwa Deodati Milanzi aliyekamatwa katika kijji cha Kikunja wilayani Songea akiwa na bunduki aina ya Gobole inayodaiwa kutumika kwenye uwindaji haramu wakiwemo Tembo.

Katika tukio jingine katika kijiji hicho hicho  cha Kikunja  Polisi inamshikilia mzee  Mganamakua Makale mzee wa miaka 78 akiwa na silaha iliyotengenezwa kienyeji ikidaiwa kutumika kwenye uwindaji haramu akiwa pia na ngozi ya mnyama ina ya Ngolombwe.