Wafanyabiashara wa samaki katika soko la kimataifa la Mwaloni, Kirumba Jijini Mwanza wameiomba serikali kupunguza viwango vya tozo na ada za leseni ili waendelee kufanya biashara zao bila kubughudhiwa ili wakuze biashara zao na kuinua uchumi wa taifa.
Wafanyabiashara hao wametoa ombi hilo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina, aliyetembelea soko hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo yanayozikabili biashara zao.