Wavuvi wadogo wadogo wa samaki aina ya migebuka na dagaa katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma wameiomba serikali kuboresha mazingira ya uvuvi ikiwemo kuwepo kwa ndege maalumu ya serikali itakayowawezesha kufanya biashara hiyo nje ya nchi kama ilivyo kwa wavuvi wa ziwa victoria hali itakayochangia ukuaji wa uchumi wao na taifa.
Wakizungumza na ITV wavuvi na wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za uvuvi katika mwalo wa Kibirizi uliopo katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma wameiomba serikali kuboresha teknolojia za kisasa za uvuvi, uhifadhi na uchakataji ili bidhaa zao zipate soko la nje ya nchi.
.
Aidha, Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Wavuvi wadogo wadogo Tanzania Bw.Fransis John amesema endapo wawekezaji wataweza kujitokeza na kuwekeza katika Ziwa Tanganyika itawezesha kuongeza pato la taifa na kuutangaza zaidi mkoa wa Kigoma.
.
Nayo, Serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi chini ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Ulimwenguni(FAO) kupitia mradi wa FISH4ACP wamejipanga kufungua fursa zilizopo Ziwa Tanganyika pamoja na kuboresha miundombinu ya sekta hiyo.