Waziri afya maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu ameagiza mpango wa taifa damu salama kuweka utaratibu wa vitambulisho kwa wachangiaji wa damu wa mara kwa mara ili kuwapa kipaumbele pindi wanapokuwa na uhitaji wa damu huku akiwasihi watu kujenga utamaduni wa kuchangia damu na kutokuwa waoga katika kupimwa maradhi.
Akizungumza katika zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya wagonjwa wa saratani katika taasisi ya Ocean Road waziri Ummy amesema kama serikali wamefunga mashine za kisasa za upimaji damu katika kanda nane na kilichobaki ni muamko kwa wananchi tu.
Aidha waziri Ummy amehimiza mchango wa vyombo vya habari katika kuhamasisha kampeni za uchangiaji damu huku akimshukuru mkurugenzi mtendaji wa ITV/Radio One Joyce Mhavile na mchango wake katika hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi wa taasisi ya saratani amesema kuna uhitaji mkubwa wanajamii kubadili mfumo wa maisha kukabiliana na ugonjwa huo ambao wagonjwa wake wanakuwa na upungufu wa damu. 42.