Back to top

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa azigeuzia Kibao mamlaka za maji nchini

12 September 2019
Share

Waziri MKuu wa Mhe.Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka za maji nchini kote kuhakikisha hazi watozi gharama za maji wananchi kwa bei ambazo ni za juu kiasi kwamba baadhi yao wanashindwa kulipia.

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali mbalimbali ya papo kwa papo ambapo Mhe.Mariam Kisangi mbunge wa viti maalum mkoa wa Dar es Salaam aliyetaka kujua serikali inafanya nini kudhibiti bei za maji.

Mhe.Majaliwa ameongeza kuwa mamlaka za maji zipo kuwahudumia wananchi siyo kuongeza ugumu wa maisha na hivyo zihakikishe kuwa wanapanga bei za maji kulingana na hali halisi.

Amesema mamlaka zote za maji nchini zinapaswa kupitia upya bei zao na kabla ya kufikia muafaka  lazima ziwashirikishe wadau wote wakiwemo watumiaji wa huduma ya maji.

Kuhusu hali ya chakula nchini Mhe.Majaliwa amesema ni salama japo ipo baadhi ya mikoa ambayo hawakupata mavuno ya kutosha.

Hivyo kiongozi huyo wa serikali bungeni amesema wafanyabiashara nao watumie fursa hiyo kuchukua chakula sehemu ambayo kuna chakula cha kutosha kupeleka sehemu yenye uhaba wa chakula Waziri Mkuu amegusia pia ununuzi wa zao la Pamba ambapo amesema mikakati mbalimbali inaendelea kufanyika na hivyo wakulima wasijali Pamba zote zitanunuliwa.