Back to top

Waziri wa Nishati amshusha cheo msimamizi umeme Mitambo ya Kinyerezi

01 August 2019
Share

Waziri wa Nishati Dkt.Merdad Kalemani amemshusha cheo msimamizi wa nguzo kubwa za umeme katika mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi kutokana na kutoridhishwa na taarifa ya hitilafu ya umeme iliyotokea asubuhi ya Agosti moja na kusababisha taaruki kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kutembelea nguzo hizo zilizo umbali wa Kilomita moja kutoka kituo cha Kufua Umeme cha Kinyerezi, Dkt.Kalemani amesema serikali haiko tayari kufanyakazi na watendaji wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.

Akielezea tatizo liliotokea Mhandisi Msimamizi aliyoteuliwa na Dkt.Kalemani kushika nafasi hiyo, ameahidi kutafuta umbuzi wa hitilafu ya umeme haraka iwezekanavyo.

Aidha Dkt.Kalemani ametembelea kituo cha Shirika la Umeme Tanzania Ubungo ambapo ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo  kuwasilisha taarifa ya maelezo ya kuungua kwa moja ya mitambo katika kituo hicho pamoja na kuunda timu maalumu kufuatilia tatizo la kuungua mara kwa mara kwa baadhi ya mitambi ili serikali ichukue hatua.