Back to top

Zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya Heroin yakamatwa Lindi.

24 April 2021
Share

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na kikosi cha wana maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania wamekamata zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya Heroin.

Dawa hizo zimekamatwa eneo la Kilwa Masoko katika Bahari ya Hindi zikisafirishwa kwa kutumia Jahazi la Al Arbo.

Katika tukio hilo, watuhumiwa saba wamekamatwa ambao ni
 Jan Mohammad Miranira (Nahodha )., Amir Hussein., Yusiph bin Hamad., Salim Bin mohammad., Ikbal Pakir mohammad.Jawid Nuhan Nur Mohammad., Mustaphar Nowani Kadirbaksh.