Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi. Baraka Mwambage, amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa miradi tisa ya kimkakati Mkoani Pwani ikiwa ni pamoja ile ya kipaumbele ikiwemo ujenzi wa barabara ya Kibaha – Chalinze - Morogoro Expressway (km 210); Sehemu ya Kibaha - Chalinze (km 118).
Mhandisi Baraka amesema miradi mingine inayotekelezwa na Serikali kupitia TANROADS ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ni barabara ya Chalinze - Utete (Km 354.9) inayounganisha Mikoa ya Kaskazini na Kusini bila kupitia Mkoa wa Dar es salaam, barabara ya Makurunge – Saadani -Tanga (Km 178) ni barabara ya Afrika Mashariki ya kuunganisha Mkoa wa Pwani na Tanga, km 14 zipo Mkoa wa Pwani na ujenzi kwa upande wa Mkoa wa Tanga mkandarasi yuko kazini.
Nyingine ni barabara ya TAMCO - Mapinga (Km 23), barabara ya Kisarawe - Maneromango (Km 60), Maneromango -Vikumburu – Mloka – JNHPP (Km 198.71), Njia rahisi na fupi ya kufika Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere kutokea Dar es Salaam, barabara ya Kiluvya - Mpuyani (19.8Km), barabara ya Kilindoni - Rasmkumbi (52.3Km), baraara ya Ikwiriri - Mkongo2 (Km 27.74), barabara ya Mkuranga - Kisiju (Km 45) na barabara ya Kibiti - Mloka (Km 100.18).
Pia kuna barabara ya Bungu - Nyamisati (Km 40.3), Mlandizi - Maneromango (Km 65), barabara ya Mlandizi - Ruvu Jct-Ruvu SGR (Km 23), barabara ya Msoga-Msolwa (Chalinze Bypass)(Km 10) na kwamba kazi nyingine zinaendelea kutekelezwa na Serikali kupitia TANROADS ikiwemo Uwekaji wa Taa za barabarani maeneo mbalimbali.
Mhandisi. Baraka Mwambage ameeleza kuwa ukarabati mkubwa wa barabara ya zamani ya Mororgoro unaendelea kufanyika kuanzia maeneo ya Sheli - Picha ya Ndege - Misufini - Ruvu JKT – Ruvu Relini – Mzunguko wa Vigwaza – Chalinze - Mdaula na uwekaji wa taa za kuongozea magari unaendelea maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.