Back to top

WATU 9 AKIWEMO MAKAMU WA RAIS WA MALAWI WAFARIKI DUNIA

11 June 2024
Share

Watu wote tisa waliokuwemo katika ndege iliyombeba Makamu wa Rais wa Malawi Dkt.Saulos Chilima wamefariki dunia baada ndege hiyo kuanguka katika msitu wa Chikangawa.

Kafuatia ajali hiyo, Rais Lazarus Chakwera wa nchi hiyo ametoa pole kwa familia za marehemu na kutangaza bendera zote nchini humo zipeperushwa nusu mlingoti mpaka marehemu watakapozikwa.

Ndege hiyo ilianza safari zake saa tatu asubuhi jana kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Lilongwe kuelekea mji wa Mzuzu, lakini ilipoteza mawasiliano ilipofika maeneo ya milimani, Kaskazini mwa nchi hiyo na kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mzuzu  kama ilivyotarajiwa.

Dkt.Chilima amekuwa Makamu wa Rais wa Malawi tangu mwaka 2020.