Back to top

SILAA AANZISHA MIKOA MIWILI YA ARDHI PWANI

05 July 2024
Share

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa, amesema Wizara yake imefikia maamuzi ya kuanzisha mikoa miwili ya Ardhi katika Mkoa wa Pwani, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa JMT ,  Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, katika falsafa yake ya Maridhiano, Kujenga upya nchi, Uvumilivu na Mageuzi.

Waziri Silaa amesema hayo katika ufunguzi wa kliniki ya Ardhi Bagamoyo, kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za migogoro ya ardhi kwa wananchi, iliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Majengo.

Mikoa mipya iliyoanzishwa ni Pwani Kaskazini, wenye Halmashauri ya Kibaha, Chalinze na Bagamoyo na mkoa mwingine ni Pwani Kusini wenye Halmashauri za Mkuranga, Kisarawe, Mafia na Kibiti.
Katika hatua nyingine Waziri Silaa amebainisha kuwa kwa sasa Kampeni yake ya Kliniki za Ardhi zinazoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini zitafahamika kwajina la Samia Ardhi Kliniki. 

Aidha, Waziri Silaa amesema kuwa ofisi za Ardhi zote nchini zinapaswa kutoa huduma kwa uwazi na sio kutoa huduma kwa kujifungia kwenye majengo ili  wananchi waweze kusikilizwa pasipo kificho.