Back to top

WAGONJWA 762 WAHUDUMIWA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA BMH

04 October 2024
Share

Waziri wa Afya Mhe. Nassor Mazrui amehitimisha Kambi Maalumu ya Magali yenye vyumba vya upasuaji (theater) iliyo kuwa ikifanywa na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa kutoka Dodoma, kuanzia tarehe 26/09/2024 hadi 04/10/2024.

"Naifunga kambi hii nikitambua imetupa faida nyingi kwanza wananchi wa pembezoni wamepata huduma za matibabu na upasuaji, pili mmewajengea uwezo wataalamu wetu na tatu kwa kuleta magari haya nasi tunaona kunahaja ya kuwa nayo hivyo tutafanya tathimini ya kuona uwezekano wa kuwa na magari kama haya" Amesema Mhe. Mazrui

Ameongeza kuwa sasa imefika wakati wa kurasimisha mahusiano na Hospitali ya Benjamin Mkapa

"Kabla ya mwezi Disemba lazima tuje kuitembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa , nia ni kuiona na pia kuingia makubaliano rasmi na Hospitali ya Benjamin Mkapa" amesema Mhe. Mazrui ambayo yataboresha huduma za kibingwa, mafunzo na kubadilishana uzoefu wa Watalaamu. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi amezishukuru sana serikali za JMT na SMZ kwa  kutoa baraka za kambi hiyo na kuwapokea watalaamu, kuandaa mazingira  mazuri na ambapo pia mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa sana. 

"Mpaka kufikia leo mchana tumeona Wananchi 762 na katika hao 60 wamefanyiwa Upasuaji, kambi hii imekuwa na msaada kwa wakazi wa Zanzibar" alisema Prof. Makubi. Aidha, baadhi ya wagonjwa walimuomba Mheshimiwa Waziri wa Afya kuona namna ya kuongeza muda wa kambi hizo kwa siku zijazo ili Wananchi wengi wanufaike. Huduma za upasuaji ubingwa za ubongo, mifupa, macho  na njia ya mkojo zilitolewa kwa Wananchi walioko pembezoni mwa mji wa Unguja. 

Aidha, Prof. Makubi ameeleza nia ya kuja kutoa huduma Zanzibar”Sisi wote ni watanzania hivyo tunakila sababu ya kutoa huduma Zanzibar na bara , Hospitali ya Benjamin Mkapa inajukumu la kuwajengea uwezo Madaktari na Wataalamu wa Hospitali zilizopo Tanzania" amesema Prof. Makubi 

Kambi hii ya magari maalumu yenye vyumba vya upasuaji (theater) yameanza kutoa huduma Zanzibar kisha yatakwenda Dodoma,Kigoma na Burundi.