Back to top

STAKABADHI ZA GHALA ZIMEONGEZA THAMANI YA MAZAO

05 July 2024
Share

Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zakaria Mwansasu ,amesema mfumo wa Stakabadhi ghalani umechangia kuongeza thamani ya mazao na kuwezesha kupata bei zenye ushindani zinazoleta tija na faida kwa Wakulima.

Ameyasema hayo alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwenye Maadhimisho ya Ushirika Duniani ,yanayofanyika katika Viwanja vya Ipuli, Mjini Tabora.

Amesema hadi kufikia Machi 2024, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala imeratibu ukusanyaji wa mazao kilogramu milioni 371 yenye thamani ya shilingi Bilioni 905.

Kwa upande wake Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, ametoa wito kwa Wanaushirika kukusanya mazao yenye ubora ili kuepusha usumbufu kwa wanunuzi na Mfumo mzima wa Stakabadhi ya Ghala.