Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watuhumiwa wawili baada ya kuwakamata na bunduki mbili zinazodaiwa kutumika kufanyika Ujangili wakiwemo Tembo na Nyati.
Katika tukio la kwanza kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi anasema wanamshikilia mtuhumiwa Deodati Milanzi aliyekamatwa katika kijji cha Kikunja wilayani Songea akiwa na bunduki aina ya Gobole inayodaiwa kutumika kwenye uwindaji haramu wakiwemo Tembo.
Katika tukio jingine katika kijiji hicho hicho cha Kikunja Polisi inamshikilia mzee Mganamakua Makale mzee wa miaka 78 akiwa na silaha iliyotengenezwa kienyeji ikidaiwa kutumika kwenye uwindaji haramu akiwa pia na ngozi ya mnyama ina ya Ngolombwe.