Back to top

BADO MITA 2, DARAJA LA MAGUFULI KUKAMILIKA

17 September 2024
Share

Waziri wa Ujenzi, Mhe.Innocent Bashungwa, amekagua na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa  Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi), lenye urefu wa Kilometa tatu linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria, ambapo ameeleza bado sehemu ya Mita mbili ili daraja lote liweze kuunganishwa.

Ameeleza mkoani Mwanza wakati akikagua Ujenzi wa daraja hilo unaoenda sambamba na ujenzi wa barabara unganishi zenye jumla ya kilometa 1.66 upande wa Kigongo na  Busisi.

"Nimetembea kilometa tatu za Daraja la J.P Magufuli kujionea kazi, nimejiridhisha tumebakiza mita mbili (hatua mbili za miguu), ndicho kipande kilichobaki kukamilisha ujenzi wa kilometa tatu za daraja hili pamoja na barabara za maungio kiliometa 1.66 ambazo pia Ujenzi uanendelea" Mhe.Bashungwa.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa ujenzi wa Daraja la JP Magufuli, Mhandisi Abdulkarim Majuto, ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 90.5 na kazi zinaendelea kufanyika usiku na mchana, ambapo matarajio hadi kufikia mwanzoni mwa Mwezi Oktoba 2024, Daraja hilo litakuwa limeunganishwa.