Back to top

WATENGANA BAADA YA SAA 14 ZA UPASUAJI

18 September 2024
Share

Wasichana pacha wenye umri wa mwaka mmoja, walioungana kichwani, wametenganishwa kwa mafanikio makubwa wakati wa operesheni ya saa 14 nchini Uturuki, na kuongozwa na daktari bingwa wa upasuaji kutoka Uingereza.

Profesa Noor ul Owase Jeelani kutoka Hospitali ya Great Ormond Street, alitumia teknolojia bora ya kisasa iliyopewa jina la ‘mixed reality’ kukamilisha hatua ‘tata’ ya kuwatenganisha Minal na Mirha.

Minal na Mirha kutoka Pakistani, walizaliwa wakiwa wameunganisha vichwa vyao pamoja na kugawana mishipa muhimu ya damu na tishu za ubongo.

Wote wawili wanaendelea kupata nafuu hospitalini, na wanatarajiwa kupata nafuu kamili na kuishi maisha ya kawaida watakaporejea nyumbani kwao Pakistan mwezi ujao.

Operesheni hiyo katika Hospitali ya Jiji la Ankara Bilkent nchini Uturuki,  ilianza Julai 19, ambayo ilijumuisha timu ya wauguzi wa ndani, ilihitaji hatua mbili za upasuaji na ilikamilika kwa muda wa miezi mitatu, na upasuaji wa mwisho ulichukua masaa 14.

Wasichana hao mapacha walioungana walitengana baada ya upasuaji wa saa 14 ambapo kwa mara ya kwanza madaktari wa upasuaji wa Uingereza walitumia teknolojia iliyopewa jina la ‘mixed reality’  kuwasaidia kujiandaa kwa upasuaji huo mgumu.