Back to top

WANANCHI WAKABIDHIWA HATI ZA HAKIMILIKI, MSOMERA

21 September 2024
Share

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imekabidhi Hati za Hakimiliki za Kielektroniki, kwa wananchi waliohamia Msomera kwa hiari, wakitokea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wale waliokuwepo katika Kijiji hicho kabla.

Akikabidhi Hati za Hakimiliki kwa wananchi hao wa Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasisitiza kutoyauza maeneo yao na badala yake wayatunze kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Waziri Ndejembi amesema Serikali inatekeleza mradi wa kujenga nyumba, na kuwapatia mashamba wananchi, wanaohama kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, kwenda Vijiji vya Msomera, Lengusero, Saunyi na Kitwai ‘B’ vilivyopo katika mkoa wa Tanga.